|
UNAKUMBUKA HII?

Ikiwa wewe ni mpenzi wa nyimbo za Injili kwa hakika Kwaya ya Mapigano Ulyankulu kutoka Tabora sio ngeni masikioni mwako, Albamu yao iliyoitwa MWENYE MAMLAKA ilitamba sana katika miaka ya 90, nyimbo kama "Siku ya kutaabika", "Safari yao wana Israeli" na "Yesu akawaambia wanafunzi" zinaifanya Albam hii isichuje! hakika utakubaliana nami kwamba bado wanabamba!
Mwenye Mamlaka ina jumla ya nyimbo 13, toka miaka ile hadi leo toleo hili halikatiki mtaani, pata copy yako fasta! |
Album zilizoingia sokoni hivi karibuni, tembelea duka la kanda za kikristo lililo karibu na wewe ili kupata copy yako
UPENDO NKONE
anakuletea
Album iko mtaani, check duka lolote la vitabu na wauzaji wa nyimbo za kikristo ili kupata "copy" yako
kumbuka kununua original copy
|
Ikiwa wewe ni kijana na umeokoka, wewe tayari ni mtumishi wa Mungu, kama utamtumikia Mungu, mali na pesa yako vitakutumikia, hutavitumikia! Pesa bila Mungu ni bure! shetani akikupa utajiri au ukipata pesa kwa njia ya Udanganyifu (ulagali) mwisho wake ni majuto na umaskini!
Ukifikiri kuhusu pesa fikiri haya yafuatayo:-
1) Pesa sio matokeo ya maovu (dhambi) 1Tim. 6:10 inasomeka hivi " Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi" Hivyo basi uhusiano mbaya au matumizi mabaya na pesa ndio matokeo ya uovu.
2) Usiitumikie pesa
Amani yako ikitoweka kwa vile umekosa pesa ujue kuna tatizo katika utumiaji wako au sio mwaminifu kwa hilo, ikiwa wewe ni mwaminifu kwa Mungu utaelewa jinsi ya kutumia pesa 1 Tim. 6:11 inasomeka hivi: " Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo, ukafuate haki, utaua,imani,upendo, saburi na upole. |
|
Kama wewe ni mwanamuziki wa nyimbo za injili au mshika dau katika muziki huu wa injili, karibu tuunganishe nguvu katika kuukuza muziki wetu.
Tembelea ukurasa wa "Contacts" ili kuona namna ya kuwasiliana nasi au tumia email address inayoonekana chini ya page hii.
|
MUNGU KUIPIGA TANZANIA?
Hivi karibuni nimepiata email kutoka kwa rafiki yangu,
Email ilikuwa inasomeka hivi,
"Nawaarifu ndugu zangu katika Mwili wa Yesu. Ghadhabu kuu ya Mungu imekalia taifa hili siku si nyingi zijazo. Kila atakayepata ujumbe awaarifu wateule popote waombe. Ni upendo wa Mungu kwamba hafanyi jambo kabla ya kuwaambia watu wake.
Anazo sababu kuu tatu kwa nini anaipiga Tanzania. Watu wamezubaika kwa kuwaza kiko wapi kile cha Tanzania itubu! Kiko wapi nabii zilizokuja baadaye kuhusu taifa hili! Mungu anasema hatanii ghadhabu yake inakuja, inakuja na si muda mrefu tanzania haitasalia, amani haitakuwepo
ENDELEA KUSOMA |
DAILY VERSES
DAILY QUOTES
|
Je wewe una mzigo wa kuomba? je ungependa kuiombea huduma hii? unaweza kushirikiana unaweza kuungana na katika kuombea jamii, huduma, afya, taifa n.k, tunaweza kuungana wote na kumwita Mungu kwa umoja naye atafanya.
Mambo ya kuombea
- Tuiombee Tanzania wakati huu wa Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
Posted by Mary, 8th November'05
|
- KARIBUNI WAPENDWA
Tunapenda kuwakaribisha watu wote kwa upendo wa Kristo, KARIBUNI na tujumuike wote, kwa uhuru tushirikiane kama mwili wa Kristo, usisite kuwasiliana nasi ikiwa una wazo lolote kwa ajili ya mtandao huu, au wazo kwa ajili ya jamii yetu, unakaribishwa sana
MUNGU NA AWABARIKI!
|
- Mungu Baba ~ Upendo Nkone
- Matendo yako yatisha ~ Angel Chibalonza
- Usikumbuke ~ Jane Misso
- Ulinipenda ~ Tina Marego
- Hatukutaki Shetani ~ O.B.Family
- Songa Mbele ~ Bahati Bukuku
- Hakuna Tatizo ~ Flora Mbasha
- Baba wa Mbinguni ~ Nacky Imatta
- Hapana Rafiki ~ Beatrice Mhone
- Mimi sio Mtumwa tena ~ Joshua Makondeko
Bonyeza Hapa Kupendekeza Wimbo katika chati hii
|